Ni jambo la kushangaza kuona matatizo mbalimbali yanaikummba dunia wakati wajuzi stadi katika uwanja wa diplomasia ya kimataifa wapo.Matatizo haya yanasababishwa na suala kiuchumi na siasa za dunia yaani world politics.Kwa nchi zilizoendelea hususani za magharibi diplomasia yake hutegemea sana nguvu za kijeshi na hii inajidhihirisha pale wanapotumia chombo chao mathubuti cha kujihami yaani NATO,kuhakikisha kuwa diplomasia yao ya kimataifa yenye manufaa ya kiuchumi inafanikiwa kwa nguvu za kijeshi.Wakati huohuo nchi za mashariki ya mbali kama china na zile za economic tigers hutumia nguvu za kiuchumi na bidhaa katika hali ya teknolojia ya juu kufanikisha diplomasia yao ya kimataifa, na hii pia inajidhihirisha pale wanapozalisha bidhaa nyingi haramu na sahihi yaani ubidhaaishaji [comparative advantage] na kuuza nje kwa bei nafuu.
Kwa hiyo katika kuhakikisha adhma yao inafanikiwa yaani katika kupata maeneo ya uwekezaji mkubwa wa mali ghafi, soko huru,na wafanyakazi rahisi husababisha mikwaruzano na migogoro ya kiuchumi [economic conflicts] ambayo yangeweza kusuluhishwa kidiplomasia tu [economic diplomacy].Ile nadharia ya ubinafsi imepitwa na wakati na sasa kuna utandawazi ambao ndio unaochochea matatizo duniani kwa maana isiyoeleweka[misconception and abuse of globalism] ,Diplomasia ya kimataifa imefifishwa sana na mambo haya na kufanya tathnia nzima ya diplomasia kufunikwa.Matokeo yake ni migogoro isiyoisha,vita vya kiraia na kati ya nchi na nchi,kuporomoka kwa soko la dunia [fall of world market],na kuporomoka kwa uchumi wa kidunia[international economy]nk, Nini kifanyike ni suala la nchi kuchukua hatua za kidiplomasia,katika kuhakikisha dunia inakuwa mahala pa usalama kwa maendeleo ya biashara na ustawi wa kiuchumi.
No comments:
Post a Comment